Hawa ndio wachezaji 22 walioitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars
tShirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kikosi cha wachezaji 22
kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA dhidi ya Namibia
(Brave Warriors) itakayochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek,
Namibia.
Wachezaji walioitwa katika timu hiyo ni makipa Deogratius Munishi
(Yanga), Ivo Mapunda (Simba) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki wa pembeni
ni Edward Charles (JKT Ruvu), Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili
(Mbeya City) na Michael Aidan (Ruvu Shooting).
Mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam) na Kelvin Yondani (Yanga)
wakati viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), David Luhende
(Yanga), Frank Domayo (Yanga), Jonas Mkude (Simba) na Mwinyi Kazimoto
(Markhiya Sports Club, Qatar).
Washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance Mwanza), Haruna Chanongo
(Simba), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Yanga), Ramadhan Singano
(Simba) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo- DRC).
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaingia
kambini Machi 1 mwaka huu, kwenye hoteli ya Accommondia inatarajiwa
kuondoka Machi 3 mwaka huu kwenda Windhoek.
Wachezaji ambao timu zao zinacheza mechi za mashindano ya kimataifa
na ligi wikiendi hii wataripoti kambini mara baada ya mechi zao
kumalizika.
0 comments: