PICHA:FILAMU ZA SWAHILIWOOD ZAZINDULIWA RASMI USIKU WA JUZI KATIKA UKUMBI WA CENTRUY CINEMAX - OYSTERBAY JIJINI DAR


Mkurugenzi wa Media For Development International (MFDI) – Tanzania Bw. John Riber akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Filamu tatu chini ya mradi wa Swahiliwood. MFDI inatambua umuhimu wa tasnia ya filamu (ambayo kwa sasa inajulikana kama Bongo movie), na sio tu kwamba ni daraja linaloelezea habari za kijamii, lakini pia kama tasnia am­bayo inaweza kuleta maendeleo na ajira kwa vijana wa Kitanzania.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika usiku wa kipekee kushuhudia uzinduzi wa filamu za Swahiliwood wakimsikiliza Mkurugenzi wa Media For Development International (MFDI) – Tanzania Bw. John Riber. Filamu tatu zilizozinduliwa katika usiku wa jana ni Network, Sunshine na Mdundiko.
Wakongwe katika tasnia ya filamu hapa nchini Tanzania Bw. Jacob Steven (JB) kushoto na Bw.  Muhsin Awadh (Dk. Cheni) wakiwa ukumbini tayari kushudia uzinduzi wa Filamu za Swahiliwood katika Ukumbi wa Century Cinemax – Oysterbay.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika moja ya kumbi za Century Cinemax – Oysterbay wakitazama filamu ya Mdundiko mara baada ya uzinduzi. Filamu zote zinahusu mapam­bano ya UKIMWI ambapo watazamaji watapata elimu na watengenezaji watapambana na kufanikiwa katika maswala ya kibiashara kwa kuiga muundo wa Swahiliwood.
Wadau wa Proin Promotion ambao ni wasambazaji wakuu wa Filamu zote tatu nchi nzima wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Red Carpet ya uzinduzi wa filamu za Swahiliwood.Picha Na Josephat Lukaza

0 comments: