BARAZA LA MTIHANI LATOA UFAFANUZI NA ALA,A NA MADARAJA YA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2013:
Baraza la Mitihani nchini limetoa ufafanuzi wa alama na madaraja yalivyopangwa kutokana na matokeo ya mtihani wa watahiniwa walioitimu Kidato cha Nne 2012/13 baada ya malalamiko yaliyotokana na mkanganyiko wa utaratibu huo mpya ambao haukuwepo katika miaka ya nyuma.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Mtendaji wa Baraza
hilo Dk Charles Msonde amesema utaratibu huo umelenga kupunguza
mlundikano wa alama katika kundi moja.
Sasa katika makundi yetu haya saba, kama nilivyotangulia kusema, ni gredi D ndiyo ufaulu. Kama mtahiniwa alipata gredi D na kuendelea, atakuwa amefaulu. Mtahiniwa katika somo,
Sasa mtahiniwa huyu anahesabiwa vipi kufaulu kwa ujumla wake mtihani?
Amefanya masomo mbalimbali tunampangaje katika madaraja?
Madaraja ya ufaulu, yamepangwa kwa mujibu wa kifungu cha 20, kifungu kidogo 1 – 6 cha Kanuni za Mitihani, kinachoelekeza kuwa, Ufaulu katika daraja la I – III upangwe kwa kuzingatia idadi ya alama, yaani points, na ufaulu katika daraja la IV unapangwa kwa kuzingatia ufaulu wa chini alioupata mtahiniwa ambao ni gredi D katika masomo yasiyopungua mawili au kwa kiwango kisichokuwa chini ya gredi C katika somo moja.
Aidha Dk Msonde
amesema sifa za kujiunga na mafunzo katika ngazi kwa kutumia mfumo huo
mpya wa madaraja, utatolewa na mamlaka husika, ambapo Kamishana wa Elimu
ndiye mwenye mamlaka ya kulitolea ufafanuzi.
----------------
UFAFANUZI WA MASWALI MBALIMBALI YA WADAU WA ELIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2013
Baraza la
Mitihani la Tanzania lilitangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne
(CSEE) 2013 tarehe 21/02/2014. Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo,
Baraza limekuwa likipokea maswali mbalimbali yanayoashiria kuwa baadhi
ya wadau wa elimu hawakuelewa vizuri kuhusu Viwango vya Ufaulu (grade
ranges), alama ya chini ya ufaulu (pass mark) na Ufaulu wa jumla wa
mtahiniwa (overall performance). Baraza la Mitihani linapenda kutoa
ufafanuzi katika mambo hayo kama ifuatavyo:-
1. Viwango
vya ufaulu (grade ranges) ni makundi ya alama yanayopangwa ili kuwaweka
pamoja watahiniwa wenye uwezo unaofanana katika somo husika na
kuwatofautisha na watahiniwa waliopo katika kundi jingine. Makundi haya
hupangwa ili kuwawezesha wadau kutambua namna watahiniwa
walivyotawanyika katika viwango mbalimbali vya umahiri wa somo husika.
Baraza la Mitihani la Tanzania, limekuwa likitumia makundi Matano (5)
kwa kipindi kirefu hadi mwaka 2012.
Aidha, Kuanzia
Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2013, Baraza limeanza kutumia utaratibu
wa Makundi Saba (7) ambayo ni A, B+, B, C, D, E na F. Utaratibu huu
umelenga kupunguza mlundikano mkubwa wa alama katika kundi moja.
Mgawanyo wa makundi hayo ni kama inavyoonekana kwenye Jedwali la 1.
Jedwali Na 1: Viwango vya ufaulu vilivyotumika katika Matokeo ya CSEE 2013.
Kundi
|
Gredi
|
Alama
|
Idadi ya Pointi
|
1
|
A
|
75 - 100
|
1
|
2
|
B+
|
60 - 74
|
2
|
3
|
B
|
50 - 59
|
3
|
4
|
C
|
40 - 49
|
4
|
5
|
D
|
30 - 39
|
5
|
6
|
E
|
20 - 29
|
6
|
7
|
F
|
0 - 19
|
7
|
Aidha, Idadi ya
makundi ya ufaulu hutofautiana kati ya nchi na nchi kulingana na
mahitaji ya nchi husika. Kwa mfano; Kenya wana makundi Kumi na mbili
(12), Malawi Tisa (9), Uganda Tisa (9), Nchi za Afrika magharibi
(Nigeria, Ghana, Siera Leone na Liberia) makundi Tisa.
2. Kwa
kuzingatia viwango vya ufaulu vilivyoainishwa katika makundi saba
yaliyopo kwenye Jedwali na 1, kiwango cha chini cha ufaulu ni gredi D na
kiwango cha juu cha ufaulu ni Gredi A. Mtahiniwa atakuwa amefaulu somo
husika iwapo atapata gredi D na kuendelea. Aidha, mtahiniwa aliyepata
gredi E na F atakuwa hajafaulu somo husika.
3. Madaraja
ya ufaulu yamepangwa kwa mujibu wa kifungu cha 20 (1)-(6) cha Kanuni za
Mitihani kinachoelekeza kuwa Ufaulu katika daraja la Kwanza hadi la
Tatu upangwe kwa kuzingatia jumla ya alama (Points) na Ufaulu katika
Daraja la Nne unapangwa kwa kuzingatia ufaulu wa chini aliopata
mtahiniwa ambao ni gredi D katika masomo yasiyopungua mawili au ufaulu
kwa kiwango kisichokuwa chini ya Gredi C katika somo moja. Hivyo,
madaraja yaliyotumika ni kama yanavyoonekana kwenye Jedwali la 2.
Jedwali 2: Madaraja yaliyotumika katika CSEE 2013
4. Kwa mujibu wa
Kanuni za Mitihani, ufaulu wa somo katika Gredi A hadi C utakuwa ni
ufaulu wa “Credit” na Gredi D itahesabika kuwa ni “pass”. Aidha Gredi E
na F zitakuwa alama za kufeli.
5. Baraza
la mitihani la Tanzania linapenda kutoa taarifa kwamba ufafanuzi wa sifa
za kujiunga na mafunzo katika ngazi mbalimbali kwa kutumia mfumo huu
mpya wa madaraja utatolewa na mamlaka husika ambapo Kamishna wa Elimu
atalitolea ufafanuzi zaidi.
Imetolewa Na:
KAIMU KATIBU MTENDAJI
25 Februari, 2014
0 comments: