huyu ndiye staa wa muvi ya TITANIC alivepigwa na shabiki wake kisa kizima kipo hapa
Mwanamume mmoja amekamatwa baada
ya kumshambulia kwa makonde muigizaji maarufu duniani Brad Pitt usoni
mwake katika sherehe ya ufunguzi wa filamu ya Maleficent mjini Los
Angeles.
Mwandishi habari wa Ukraine Vitalii Sediuk -
anayejulikana kwa kuwahahadaa watu mashuhuri duniani ,aliripotiwa
kuonekana akivuka kizuizi na kumkumbatia Brad kabla ya kumpiga usoni.Msemaji wa kampuni ya Disney iliyotengeza filamu hiyo alisema kuwa walisikitishwa na kitendo hicho na kwamba polisi wanafanya uchunguzi.
Sediuk alizuiliwa na polisi Jumatano usiku akisubiri kuachiliwa kwa dhamana ya dola 20,000.
Polisi walisema kitendo cha kijana huyo kilikuwa cha maksudi ingawa uchunguzi bado utafanywa.
0 comments: