kama unampango wa kwenda Brazil kuangalia kombe la dunia stori hii inakuhusu
Mawaziri wa ulinzi nchini Brazil wameweka wazi
kuwa zaidi ya vikosi vya kijeshi laki moja na nusu (150,000)
vitasambazwa nchini humo kuhakikisha kunakuwa na usalama wa kutosha
wakati mashindano ya mwaka huu ya kombe la dunia.
Kwa mara ya kwanza mpira unarejea katika ardhi yake ya nyumbani kwa
zaidi ya miaka 60 wakati Brazil ikiwa katika maandalizi ya mwisho ya
kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa zaidi duniani ambapo kwa kiasi
fulani hali ya usalama imeonekana kuwa si nzuri kufuatia maandamano ya
hapa na pale.Kumekuwa na maandamano ya wananchi wenye hasira wasiotaka mashindano hayo yafanyike, wengi wamekuwa na hasira juu ya kiasi cha pesa kilichotumika kwa ajili ya maandalizi yake zaidi katika kipindi ambacho nchi inakabiliwa na mtikisiko wa kiuchumi.
0 comments: