kama ulikuwa unatamani kushiriki Shindano la Big brother Africa hii inakuhusu





Screen Shot 2014-05-26 at 6.11.50 PM
Unaambiwa shindano hili ambalo limekua likifanyika na kuhusisha Watanzania toka lilipoanza ambapo ni Mtanzania mmoja tu (Richard) ndio alichukua ushindi katika miaka yote hiyo ya ushiriki.
Ilizoeleka shindano huwa linaanza mwezi May lakini la mwaka huu 2014 kutokana na kombe la dunia, litaanza September 7 ikiwa ni season 9 ambapo time hii idadi ya nchi zinazoshiriki ni ileile ya nchi 14 ila kuna nchi moja imeondolewa.
Angola wameondolewa na sasa Rwanda wameingizwa kwa mara ya kwanza huku nchi nyingine zitakazoshiriki zikitajwa kuwa niBotswana, Ethiopia, Ghana, Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Sierra Leone, Rwanda, South Africa, Tanzania, Uganda, Zambia and Zimbabwe.
Screen Shot 2014-05-26 at 6.13.45 PMWashiriki wote ni kuanzia walio na umri wa miaka 21 ambao ni lazima wawe ni Wananchi wa hizo nchi zenyewe na wawe na hati za kusaifiria kutoka nchi hizo.
Tarehe za kuwasaka washiriki wa mwaka huu zitatangazwa June ambapo kwa stori nyingine kuhusu BBA ya mwaka huu zitatoka mwezi ujao.
Kuhusu shindalo litakavyokuwa unaambiwa Biggie ndio atawasuprise watazamaji.

0 comments: