Picha 10 za gari analotembelea H.baba kwa sasa
Maisha ya mastar wetu wa Kitanzania yanazidi kukua zaidi na kuwapelekea kumiliki baadhi ya vitu vya gharama kutokana na jitihada zao na kujipanga vizuri na kuepuka kulewa sifa.
Leo kwenye Exclusive na AyoTV na millardayo.com mume wa Flora Mvungi, H Baba staa wa single za Mpenzi Bubu, Poteza na nyingine ameonyesha gari lake jipya analotembelea na kusema vyanzo vingine vya mapato ni pamoja na bidhaa zake za pipi alizozizindua miezi michache iliyopita zinazopatikana Mwanza pekee pamoja na uigizaji wa filamu mbalimbali za kitanzania.
Hii gari injini yake iko nyuma alafu buti liko mbele ambapo staa huyu anakua miongoni mwa mastaa wachache walioamua kuwa na magari ya kipekee tofauti na yale tuliyoyazoea ambayo ni mengi yanafanana.
H Baba ni staa ambae anasema jitihada za kazi zake sio tu ili atembelee magari mazuri bali aishi sehemu nzuri na aweze kusaidia wanaomzunguka na hata wasiomzunguka manake ni mtu mwenye moyo wa huruma sana.
0 comments: