Hili ndilo tamko la Wafanyabiashara na Wajariamali wa Tanzania kuhusu mashine za TRA
Jioni
ya February 2 Uongozi wa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania- JWT kwa
niaba ya wafanyabiashara na wajasiriamali umetoa taarifa kwa
wafanyabiashara wote na umma kwa ujuma kuhusu mashine za zinazotolewa na
Tra.
Wafanyabiashara
hao wamedai Serikali kupitia mamlaka ya mapato Tanzania[TRA] taratibu
za kuleta namna mpya ya ukusanyaji kodi kwa namna ya mfumo wa mashine za
kielektroniki[EFD] kumesababisha migomo sehemu mbalimbali
nchini,jumuiya hiyo kupitia vyama vya wafanyabiashara vya mikoa na
maeneo mbalimbali vimefanya juhudi za kuwatuliza wafanyabiashara na
kutafuta suluhisho ndani ya Serikali kwa kukutana na idara mbalimbali za
Serikali.
Miongoni
mwa Idara hizo za Serikali ni pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania
[TRA],Mkuu wa Wilaya ya Ilala. Mh.Raymond Mush,Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam. Mh. Merk Sadik na Maofisa wa Ikulu na pia walikutana na Wizara
mbili yaani wizara ya Fedha na Uchumi pamoja na Viwanda na Biashara.
Kutokana
na vitu hivyo Jumuiya hii imetoa msimamo wao ambao wamedai bado wanayo
imani na wanasubiri tume iundwe kama walivyokubaliana na ifanye kazi
yake,kufuatia mgongano wa misimamo ya wizara mbili wameomba mamlaka
zilizo juu ya wizara hizi ziingilie kati ili kuondoa hofu kwa
wafanyabiashara kote nchini.
Pia
wameiomba serikali iwape ufafanuzi juu ya kauli sahihi ya kufuatwa na
wafanyabiashara hao ambayo ni ile ya Waziri wa fedha na uchumi kupitia
Mh. Saada Mkuya, au ya Mh Dr Abdallah Kigoda waziri wa wizara ya viwanda
biashara na masoko, ili wajue upi ndio msimamo wa serikali.
Pia Wamemuomba Mh. Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete aingilie kati suala
hili kwani linawapa mashaka kama amepewa taarifa sahihi juu ya msingi
wa madai yao ambao madai yao ni maboresho ya mfumo mzima wa ukusanyaji
kodi (Tax Regime) pamoja na uendeshaji biashara nchini.
Kwa maelezo ya wafanyabiashara hao wamedai hauendani na misingi ya
kibiashara na kupelekea nchi kuwa moja kati ya nchi inayo kimbiwa na
wawekezaji pamoja na kuwafilisi wachumi wazawa wa Tanzania kutokana na
mifumo isiyo kuwa na tija kwa wafanya biashara na yenye kuchochea
rushwa.
Wamemalizia kwa kusema endapo serikali itashindwa kutoa kauli sahihi
na suluhisho wanaamini viongozi wao wa JWT watakuwa wamefanya sehemu
yeo kwa bidii kubwa na juhudi kubwa sana kuepusha mgongano baina ya
serikali na wafanyabiashara kote nchini.
Ambapo wamesema watajitoa katika kutafuta suluhu na kuwaacha wadau
waamue njia watakayoona ni sahihi katika kuwasilisha madai yao,ambapo
jumuiya hiyo wamekuwa mstari wa mbele kuzuia migomo na mivutano baina
ya wafanya biashara na serikali huku wakitoa angalizo kwa serikali kama
hatua staiki hazita chukuliwa wafanya biashara hao wanaweza kuingia
kwenye migomo isiyo ya lazima.
source:milard ayo.com
0 comments: