WORLD CANCER DAY: SIKU YA SARATANI DUNIANI LEO FEBRUARI 4…


WORLD CANCER DAY: SIKU YA SARATANI DUNIANI LEO FEBRUARI 4…
Saratani ni moja kati ya magonjwa hatari sana duniani.

Siku ya Saratani duniani, huadhimishwa kila Februari 4 ya kila mwaka…Lengo kuu la maadhimisho ya siku hii ni kutoa elimu zaidi kuhusiana na kujikinga, kwenda kupima na jinsi ya kupata matibabu endapo utagundulika kama umeathirika na Saratani. Kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huu wa kansa kufikia mwaka 2020 ndiyo lengo kuu la Union For International Cancer Control (UICC), taasisi inayohusika na kuandaa na kuratibu siku hii duniani kwa ujumla.
Mapambano dhidi ya Saratani…Inawezekana endapo watu wote watapewa elimu ya kutosha juu ya dalili nyemelezi ambazo huashiria mwanzo za ugonjwa huu; jinsi ya kujikinga pamoja njia zipi zitumike kumpatia matibabu muathirikia wa saratani.
Taasisi ya saratani ya Ocean Road imesema inakabiliwa na wingi wa wagonjwa wanaofika katika taasisi hiyo ambapo kwa mwaka jana pekee, wagonjwa 5244 wapya walihudumiwa na taasisi hiyo. Tanzania ni miongoni mwa nchi katika Jangwa la Sahara, linalokabiliwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa saratani.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Saratani Duniani, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road ,Prof Twalib Ngoma, amesema licha ya ugonjwa huo kuwepo nchini kwa miaka mingi na kusababisha vifo vya watu wengi, bado jamii haina elimu sahihi kuhusiana na ugonjwa huo. Lakini pia Taasisi hiyo, inakabiliwa na upungufu wa vitendea kazi
Takwimu za ugonjwa wa Saratani zinaonyesha kuwa Tanzania kila mwaka wanagundulika wagonjwa wapya 21,180 na zaidi ya watu 16,000 hufarika kila mwaka kutokana na ugonjwa huo wa saratani.

0 comments: