MAKALA:MAN CITY KUSHTAKIWA KWA KUVUNJA SHERIA YA "FINANCIAL FAIR PLAY" WANAWEZA KUFUNGIWA KUCHEZA CHAMPIONS LEAGUE MSIMU UJAO
Arsenal, Chelsea na Liverpool wanaweza kutumia kipengele kidogo kwenye sheria ya "financial fair play' ya UEFA ili kuibania Manchester City haki ya kucheza katika mashindano ya Champions league msimu ujao.
Kuna kanuni za kisheria zinazowapa wapinzani haki ya kuwashtaki City kwamba wamekiuka sheria na kushindwa kufuata sheria ya ya UEFA ya ‘Financial Fair Play’ (FFP).
Inafahamika na vyombo vya habari nchini Uingereza vimeripoti kwamba wanasheria wa vilabu kadhaa vikubwa wanaelewa juu ya suala hili na wanaangalia kwa umakini ya kutumia vipengele vya sheria hiyo ili kuishtaki rasmi Man City.
Jana usiku kocha wa Chelsea Jose Mourinho, ambaye timu yake inakumbana na City kesho Jumatatu, aliituhumu timu ambayo hakuitaja jina kwa kukiuka sheria ya FFP.
Alisema: ‘Kuna vilabu ambavyo vinafuata sheria ya FFP vizuri sana lakini kuna baadhi ya vilabu vinaenda kinyume na sheria hii. Kwangu, jambo hili lipo wazi kabisa. Sisemi jina la klabu au vilabu - hiyo sio kazi yangu."
Alipoulizwa kama ni City ndio waliovunja sheria hiyo na wapo kwenye kuchunguzwa na UEFA, aliongeza: "Ni kazi ya Mr. Platini na watu wengine kujua hilo, sio yangu…Nasubiria watafanya nini."
FFP inaelekeza vilabu visipate hasara isiyozidi kiasi cha £37million kwa misimu ya 2011-12 na 2012-13 kwa pamoja, vinginevyo basi basi klabu husika itakayoenda kinyume itakumbana na adhabu ya kufungiwa kucheza katika michuano ya ulaya miongoni mwa adhabu nyingine. City wiki iliyopita walitangaza kupata hasara ya £51.6m kwa msimu wa 2012-13 pekee, kwa maana hiyo watakuwa wamepata hasara ya £149.5m ndani ya miaka miwili.
SOURCE:Shafih dauda
0 comments: