LADY JAY DEE ADAI TALAKA KWA GARDNER, SOMA KISA KIZIMA HAPA


UNAWEZA ukakataa lakini ndivyo ilivyotokea, ndoa ya mtangazaji mahiri Bongo, Gardner 
Gabriel Fikirini Habash ‘Kapteini’ na Mbongo Fleva, Judith Wambura Mbibo  
 iliyofungwa miaka 9 iliyopita inadaiwa kuingia kidudu kufuatia mke huyo kuomba aandikiwe 
talaka, ni Ijumaa Wikienda pekee lenye uthubutu wa kuripoti mkasa wote.


Mnyetishaji wa kisanga hiki, aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa mara baada ya mume huyo 
kupata mchongo mzima alirudi nyumbani akiwa na furaha na kumwambia mkewe kuhusu bahati 
hiyo.Baada ya Gardner kupata mchongo wote wa kazi alikwenda mbio nyumbani 
kwake Kimara (Dar) ili akamwambie mkewe.

Pia katika safari ya kwenda Kenya kupiga mzigo ilikuwa aende na mkewe huyo kwa sababu 
lilikuwa suala la kuhamisha makazi yao Tanzania,” kilisema chanzo hicho.


Chanzo kikatoboa kwamba Gardner alipofika nyumbani kwake na kumweleza mkewe, alikumbana 
na kitu ambacho hakukitarajia.

Komando (Jide) alihamaki na kumjia juu akisema yeye hawezi kuondoka Tanzania kwenda kuishi 
Kenya, kama Gardner analiona jambo hilo ni heri kwake, amuandikie talaka yake na kuachana 
ili kila mmoja achukue hamsini zake,” chanzo kilizidi kuporomosha maneno.
 
KWA NINI JIDE HAKUPENDA 
 Habari zilizidi kuanikwa kwamba Jide au Binti Machozi alifikia uamuzi huo baada ya 
kugundua kuwa kitendo cha kwenda kuishi Kenya kitaua bendi yake ya Machozi na sehemu 
ya biashara ya Nyumbani Lounge iliyopo Ada-Estate, Kinondoni, Dar.

MBAYA ZAIDI
Taarifa zikazidi kumiminika kwamba, mbali na Jide au Anakonda kuhofia biashara zake 
kufa, lakini pia hakupenda Gardner aondoke hata peke yake kwa sababu yeye ndiye meneja 
wa miradi hiyo miwili.

Mimi nilipopata habari hizo nilikutana na Jide nikamuuliza, akanijibu 
ameamua iwe hivyo tu, kikubwa mumewe (Gardner) aamue moja kati ya hayo mawili 
kwani yeye ana haki akiwa kama mkewe wa ndoa,” kilisema chanzo kikimkariri 
Jide. 
 GARDNER AISHIWA NGUVU 
Kufuatia majibu ya mkewe, taarifa zinasema mtangazaji huyo ambaye alishawahi 
kupiga mzigo kwenye kituo cha Radio Clouds FM cha jijini Dar alijikuta akiishiwa
 nguvu na kuachana na dili hilo mara moja.

Gardner alisalimu amri kwa mkewe, akaamua kuachana na dili la kwenda kutangaza Kenya. 
Lakini alifikiri sana akasema ni kweli kuhamia Kenya kungeua miradi yao ya Tanzania 
maana ingekosa msimamizi wa kuaminika,” chanzo kiliweka wazi.
source:http://www.swahilione.info

0 comments: