hiki ndicho alichokisema Ali Kiba kuhusu kama anaweza kufanya Collabo na Diamond
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba amesema kufanya
na msanii wa muziki huo, Naseeb Abdul Diamond Platinum& haitakuja
kutokea katika maisha yake.
Kauli hiyo ya Ali Kiba imekuja baada ya mashabiki wa muziki huo,
kumshauri afanye kazi na msaniii huyo kwa kushirikiana na msanii mwenzao Omary
Nyembo ‘Ommy Dimpoz na kuibashiri kwamba itakua kazi nzuri kutokana na vipaji
walivyonavyo wakali hao
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ali Kiba alisema amekuwa
akipokea maoni mbalimbali kutoka kwa mashabiki wake lakini hicho kitu hakiwezi
kutokea kamwe.
Kiukweli sifikirii na sidhani kama itakuja kutokea kwani kufanya kazi
na Diamond ni mfano wa kudeki bahari haitakuja kutokea kamwe, naomba wapenzi
wangu waangalie kazi nyingine nitakazotoa sio kusubiri kufanya kazi na msanii
Ali Kiba ni kati ya wasanii ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya
muziki huo kutokana na kipaji chake cha kutunga mashairi ambayo yanavutia na
Msanii huyo kwasasa anatamba na kibao chake kinachojulikana kwa jina
la ‘Kujiinamia’ ambacho ameshirikiana na mdogo wake, Abdu Kiba.
0 comments: