Hili ni ombi la Mama Mangwea kwenda kwa Maproducer wote.
Albert
Mangwea ni miongoni mwa wasanii wanaoaminika kuwa na nyimbo nyingi sana
ambazo bado hazijatoka,wakati wa kumbukumbu ya kifo cha Mangwea
Morogoro iliyofanyika November 2013 Millardayo.com iliongea na familia
yake kuhusu mpango wa nyimbo ambazo bado hazijatoka za Mangwea.
Keneth Mangwea kaka wa Marehemu Mangwea alisema wanashirikiana na
rafiki wa karibu wa Marehemu Mangwea M to The P kukusanya nyimbo kwenye
studio tofauti tofauti ambazo aliwahi fanya marehemu Mangwea na nia ni
kuziweka kwenye album moja.
Leo
kupitia XXL ya Clouds Fm Mama mzazi wa Mangwea ameomba kwa
watayarishaji wote[Producers]ambao Marehemu Mangwea amewahi kufanya nao
kazi kumletea nyimbo hizo kwa ajili ya kupata haki miliki[Copyright]Mama
mzazi katoa namba za simu ili ikitokea ukiamini unao hata wimbo mmoja
wa Marehemu umpigie.
Namba hizo alizozitoa mama ni 0754 967738,0755 303552 na 0718 592620 hii ni kama una kazi za Marehemu Mangwea.
0 comments: