WALICHOKISEMA JOH MAKINI NA NIKKI WA II JUU YA VIDEO YAO ‘NJE YA BOX’ KUCHEZWA CHANNEL O.
Jana
ilikuwa siku nzuri kwenye historia ya muziki ya kundi la Weusi
linaloundwa na wasanii watano kutoka Kaskazini mwa Tanzania, Arusha,
baada ya video ya wimbo wao ‘Nje ya Box’ kuchezwa Channel O.
Joh
Makini aka Mwamba wa Kaskazini anaamini walichelewa tu kufika hapo
walipofika, lakini pia akawashukuru wale wote waliofanikisha wao kufika
pale walipofika.
Ameeleza
pia sababu zilizomfanya achelewe kufika hapo na kudai kuwa kutokuwepo
umoja kati ya wasanii wa Tanzania kuzisukuma kazi zao ni moja ya
kikwazo, na kuutolea mfano umoja uliopo kati ya wasanii wa Nigeria ambao
umewawezesha kuiteka Afrika na kuvuka mipaka.
“Sipendi
sana kulaumu watu, lakini…unajua wenzetu Nigeria wanatupiga bao kwa
sababu wenyewe nchi nzima wanafanya kazi kama timu moja.” Joh Makini
ameieleza tovuti ya Times Fm.
Rapper huyo ameeleza pia kuhusu jinsi walivyojipanga kuendelea kumaintain level waliyofikia na mpango wa video ya wimbo wa Gere.
“Sisi
Weusi ni watu ambao tunavunja rekodi zetu, ni lazima uweze kuvunja
rekodi zako mwenyewe ili uweze kuendelea mbele. Kwa hiyo kazi yeyote
nyingine itakayokuja baada ya Gere itavunja rekodi ya Gere. Unajua Nje
ya Box imetimiza kile ambacho tuliiagiza kufanya. Kwa hiyo hatuwezi
kubaki kwenye Nje ya Box siku zote.
“Nyuma ya
Nje ya Box kuna Bei ya Mkaa Video inakuja, kuna Nikumbatie..zote
tunaamini zitakuwa na impact tofauti na kazi zilizopita nyuma.”
Amefunguka Joh.
Joh na Nikki wa Pili walieleza jinsi ambavyo waliweza kufanikisha kuifikisha Nje ya Box Channel O hadi kupata air time.
“Tulipewa tu connection…kuna mdada alitusaidia tukatafuta connection
ya kule akatuma na jamaa wakatutumia form yao tukajibu.” Nikki wa Pili
ameeleza.
“Tukatuma
kwa email kwa wahusika wanaofanya kazi Channel O, wakaipokea
wakaiangalia wakajibu Email kwamba hii kazi tumeipokea na tumeikubali
itachezwa hapa Channel O. kwa hiyo I’ts possible, yaani inawezekana
kabisa. Cha msingi inatakiwa ianze pale ambapo unafanya video yako
mwenyewe kwa sababu wenzetu kule duniani hawashangai tena quality katika
hiyo level, kwa sababu quality kila mtu anayo. Lakini ndani ya quality
umeweka creativity gani ili mtu aweze kupenda kuitazama kazi yako?” –
Joh Makini.
0 comments: