Hii ni mpya kuhusu sakata la usajili wa Neymar FC Barcelona
Uchunguzi
unaoendelea wa sakata la usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil
Neymar kwenda Barcelona umesimamishwa baada ya FIFA kukataa kuwasilisha
baadhi ya vielelezo kwa ajili ya kesi hiyo kuendelea.
Jaji a mahakama moja nchini Spain Pablo Ruz alitoa ombi la ushahidi
wa vielelezo kadhaa vinavyohusisha uhamisho huo wa Neymar kutoka Santos
kwenda Catalunya, vielelezo hivyo vilikuwa vinahusisha hati kadhaa
kutoka FIFA pia mkataba wa Neymar na kampuni ya N&N (kampuni
inayomilikiwa na wazazi wa mchezaji), mkataba wake na pamoja na hati
zingine za masuala ya kifedha kutoka kwenye kampuni ya Deloitte.
Hata hivyo uchunguzi huo ulishindikana kufuatia FIFA kukataa kutoa
taarifa hizo zilizohitajika wakisema ni vitu vya siri na inabidi
vikachukuliwe kwenye mamlaka za nchi ya Uswis yalipo makao makuu ya
FIFA.
Jaji Ruz sasa atatuma barua kwenda kwenye mahakama nchini Uswis
kuomba msaada wa kupatiwa vilelezo vya ushahidi vinavyohitajika, jambo
linawekana kufanikiwa.
Sakata la usajili wa Neymar tayari limemuondoa Sandro Rossell katika
urais wa klabu ya FC Barcelona, baada ya kufunguliwa kwa kesi ya
matumizi mabaya fedha yaliyolizunguka suala la uhamisho wa mchezaji
huyo.
0 comments: