hii ndiyo makala aliyoandika Nikki wa II kuhusu thamani ya sanaa bongo.
Hii makala imeandikwa na rapper Nikki wa II, ukishaisoma unaweza kusema chako chochote…
Anaanza kwa kuuliza >>>> thamani ya sanaa ni KIKIII? ? ?
Nakutana na wasaniii wachanga wengi, Kwenye show, mitandaoni, mtaani, studio na wengine wananipigia
Wengi huomba kolabo, ushauri, namba za simu za watu mbali mbali wa Kwenye industry hii
80% huomba ushauri wa kutoka, kolabo kwa dhana ya kuwasaidia
kujulikana mapema, ama kusaidiwa kufikisha cd zao kwa watu Fulani
Fulani.
Ni Ngumu sana kukutana na msanii mchanga akakuuliza namna ya
kuboresha uwezo wake wa ku rap, kuimba ama kuwa mwandishi mzurii…kwa
kifupi kuwa msanii bora
Msanii wa kwenda Kwenye concert anataka kwenda studio, msanii Ana
nyimbo Moja na nusu Ana taka umtafutie Dili ya kurekodi….Mimi mpaka
naenda studio nilikuwa nishaperfom matamasha mengi ya kushindanisha
vipaji na nilikuwa na nyimbo mbili mpya kila wiki hazikuwa Kali ila ndio
zilikuwa hatua za kujifunza ku rap na kuandika mashairi.
Wakati natafakari nini msingi wa Sanaa kuonekana rahisi namna hii na
kua maarufu kuwa ndio inspiration kwa wasaniii wachanga na wala sio
usaniii bora…nikawasha TV Mara nikaona nyimbo ya kiwango sawa kabisa na
jamaa Mmoja ananiimbiaga nikienda saloon,
ikafuata nyingine na nyingine za aina hiyo
ikafuata nyingine na nyingine za aina hiyo
Theni ikaja interview mtangazaji anamuuliza msanii kwa nin mziki
haulipi?? Nikacheka utalipaje wakati ni kitu rahisi sana nikitoka nje tu
hapo nakipata, na hata mfanya kazi wako wa ndani anaimba sawa tu na
unaye muona kwenye TV. hamna kitu kisicho na thamani kinacholipa….kitu
ambacho sina uhakika ni Kama na yeye akiwa gheto kwake huwa Ana angalia
play list anayoipangaga
Nibiashara Binafsi sio sahihi kumjaji MTu kwa anachofanya…lakini je
haujiskii furaha kipindi ulikuta una fans 200 ukafanya wakawa 2000 loyal
fans, hautajisikia furaha kizazi kinachofuata nao wakaja kalia kiti
hicho. Biashara zetu ni binafsi lakini Jamii yetu sio na nijukumu letu
la ujumla kuandaa mazingira bora kwa watoto na wadogo zetu.
Any way turudi Kwenye mada, natafakari watu Kama kendrik lamar, 50
cent, iliwachukuwa si chini ya miaka 10 kufika mainstream, kina keri
hillson miaka 5 yakuwa backup singer, nikakumbuka mfuko wa joh makini
uliokuwa umejaa mashaiiri tumeutundika pale sebleni kwetu.
Nikakumbuka kuwa gemü ya mziki wa kizazi kipya ina Kama miaka 15 ila
ina zaidi ya wasanii 50 walio wika na kupotea wakati NAs, snoop, jay z
wana karibia miaka 20 Kwenye gem on top. Radio Kama hot 97 na host Kama
funk master flex toka miaka ya 90 mpaka Leo wanakimbiza New York, source
magazine, alafu nawaza baadhi ya vipind vikubwa vilivyo poteza umaarufu
hapa bongo, shows za TV ambazo nilikuwaga naziota kuwepo, sikumbuki
Mara ya mwisho nimeaangalia lini
Shows za kujaza diamond jubilee, msanii mmoja ndio alikuwa na thamani ya show Moja ya club Leo ni wasanii 8.
Thamani…value…hujengwa na nini?………na hujengwa na nani?,…….na
unawezaje kuilinda kulingana na mabadiliko ya muda na tamaduni za
kinyakati?………..towa maoni yako uki ya elekeza kujibu maswali hayo…..
Unaweza niandika on my twitter account Nick mweusi @nikkwapili ama on Instagram @nikkwapili
0 comments: