Wataalam waeleza jinsi picha za "Selfie" zinavyoweza kuathiri afya ya akili (mental health)
Kuongezeka kwa joto, madawa ya kulevya na rushwa ni miongoni mwa matatizo yanayoiathiri
dunia lakini kwa mujibu wa idara ya afya ya akili ya Thailand, tatizo jingine kubwa
linaelekea kuwa tishio kwa maeneo ya nchi – selfie.
Jumapili, daktari wa masuala ya akili, Dr. Panpimol Wipulakorn aliwaonya vijana wa
Thailand wanaopost picha zao wenyewe kwenye mitandao ya kujamii lakini kushindwa kupata
mrejesho chanya (positive feedback) wanakutana na matatizo ya kihisia.
Kama wakijisikia hawapati likes za kutosha kwa selfie zao kama walivyotarajia, huamua
kuweka nyingine, lakini bado hawapati majibu ya mazuri, alisema.
Hii inaweza kuathiri namna wanavyofikiri. Wanaweza kupoteza kujiamini na kuwa na mtazamo
hasi kwa wao wenyewe kama vile kujihisi wana kasoro.
0 comments: