KANUSHO LA Mh. LOWASSA KUHUSIANA NA UMILIKI WA KURASA ZA MITANDAO YA JAMII.


Kumekuwa na kurasa (accounts) mbalimbali zenye jina la Mh. Edward Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mitandao ya kijamii Kama vile Facebook,Twitter,Instagram nk.

Zinazoonye kuwa mmiliki wake ni Mh. Edward Lowassa.

Ukweli ni kwamba hizo kurasa zote hazimilikiwi na Mh. Lowassa.

Kwa maana hiyo chochote kinachoandikwa au kuchapishwa kwenye kurasa hizo,hazihusiani kwa namna yoyote na Mh. Lowassa. 

Hata hivyo Mh. Lowassa anawashukuru wote wenye kumiliki account hizo bila ya ruhusa yake, kwani anaamini wamesukumwa na mapenzi yao kwake.

Imetolewa na 
Ofisi ya Mh. Edward Ngoyai Lowassa 
Mbunge wa Jimbo la Monduli.

0 comments: