KALI YA LEO: KUTANA NA SHABIKI NAMBA 1 WA BOTAFOGO ALIYEJICHORA TATTOO 83 KUHUSIANA NA MAPENZI YAKE KWA KLABU HIYO
“Nilizaliwa mjini Botafoguense,” anaelezea Delneri Martins Viana, 69, mwanajeshi mstaafu.
Alikuwa huku akiwaangalia wachezaji kama vile Manga, Nilton Santos, Didi, Zagallo, Quarentinha, Garrincha na Amarildo kundi la wachezaji wa kikosi kizuri kuliko vyote katika historia ya klabu hiyo, baada ya hapo akawashuhudia akina, Paulo Cesar Caju na Jairzinho, baadae akashuhudia kikosi cha Botafogo kilichokuwa kikiongozwa na Tulio Maravilha kikipata mafanikio makubwa mnamo mwaka 1995.
Delneri alijichora tattoo ya kwanza - ikiwa kama kumbukumbu ya Garrincha – miaka 14 iliyopita. Baada ya hapo akaanza kunogewa na kuingiza wino mwilini mwake.
Mwili wake sasa umezungukwa na tattoo za kauli mbiu za Batafogo, majina ya wachezaji wa zamani, beji na hata Biriba, mbwa ambaye Raisi wa zamani wa klabu hiyo Carlito Rocha alivunja sheria za klabu zilizokataza wanyama - yeye alikuwa akiingia nae uwanjani akiamini ataleta bahati kwa klabu.
Alama iliyopo nje ya nyumba ya Delneri anayoishi na mkewe Marina Gonalves, na mbwa aliowapa majina ya Garrincha na Loco Abreu, iliyopo eneo la Bangu, ndani ya jiji la Rio de Janeiro, inasomeka: ‘Karibu……lakini tafadhali usiongee vibaya kuhusu Botafogo.’
Delneri anajaribu kwenda kwenye kila mchezo wa Botafogo - nyumabani na ugenini - mara nyingi akiwa anasindikizwa na watoto wake wa kike Glaucia and Marcela.
0 comments: