HII NDO HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA ASERNAL


Arsene Wenger amesisitiza pamoja na kwamba Julian Draxler hatoweza kusajiliwa Arsenal leo katika siku ya mwisho ya usajili barani ulaya, lakini na ana uhakika wa asilimia "80" kwamba klabu yake itatangaza usajili mpya leo hii.

Kumekuwepo na taarifa kwamba kcha huyo yupo sokoni akiwinda saini za wachezaji kama Miroslav Klose au Alvaro Morata baada ya uhamisho wa kumleta Julian Draxler kuonekana kuwa mgumu, lakini inaaminika kocha huyo anaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Southmpton Morgan Schneiderlin.

Kocha huyo mfaransa alikuwa akiongea na waandishi wa habari hivi punde amesema kwamba klabu yake itamkosa kiungo wao tegemezi Aaron Ramsey kwa wiki sita baada ya kupata maumivu mwezi uliopita.

"Ramsey atakuwa nje kwa wiki nne mpaka sita, nahesabu sita," aliwaambia waandishi wa habari. "Tupo kwenye jitihada za kusajili mchezaji mwingine kutokana kutokuwepo kwa Ramsey na Flamini ambaye kasimamishwa.


"Nina uhakika tutasajili mchezaji mmoja leo. Kuna asilimia 80 za kukamilika kwa suala hilo."

0 comments: