huu ndo mpango Lamar wa kununua ‘private jet’
Kila mmoja ana ndoto zake za kuwa na kitu cha thamani maishani lakini ndoto aliyonayo
producer Lamar, kwa wengi inaweza kuonekana kama kubwa mno kwake. Lamar ameiambia East
Africa Radio kuwa ana mpango wa kununua ndege yake binafsi atakayoitumia kuzunguka popote
anapotaka.
Kuonesha kwamba anataka kuanza kuishi ndoto hiyo mapema iwezekanavyo, Lamar ameshaanza
kufanya mazungumzo na wauzaji wa ndege hizo ili ajipatie yake mapema.
Lamar si mtu pekee mwenye ndoto ya kumiliki ndege binafsi. AY pia ameamua kujifunza
urubani kwa kuamini kuwa siku moja anaweza naye anaweza kumiliki yake mwenyewe.
Wanakuambia dream big, thing big. Fikiria kitu ambacho ni kikubwa zaidi ya uwezo wako.
Kwahiyo naweza kusema kuwa kila kitu kinawezekana kwasababu hata wale wenye private jet
wakati wakiwa wadogo au wakati hawawezi kuafford walikuwa wanafikiria kuwa kuna siku nao
wanaweza kuwa na private jet, so vyote viwili vinawezekana,” AY aliiambia Bongo5
wenye.
source:Bongo5
0 comments: