makala fupi Kuhusu mpango wa TFF kutaka kubadili jina la Taifa Stars

taifa-13 Jina la utani la timu ya taifa ya soka  ya Tanzania  ‘Taifa Stars’ limeonekana kuwa njiani kuachwa kutumika baada ya raisi wa TFF  Jamal Malinzi kusema kwamba wanakaribisha wazo la kubadili jina.
Katika kipindi cha maswali na majibu kilichofanyika jumanne iliyopita, TFF  kupitia Raisi wake ilisema kwamba taratibu za mwanzoni tayari zimeanza.
Utaratibu mzima utahusisha jamii. Umma utatumika katika kutoa mawazo ya jina jipya kupitia SMS.
Suala la kutaka kubadili jina kwa hakika litaleta mjadala kwenye jamii. Kwa muda mrefu kumekuwepo na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiliponda jina hilo wakisema limekaa kitaratibu na halitishi.
source:milard ayo

0 comments: