Huu ni mwisho wa Ipod? Mauzo ya kifaa hicho cha kusikilizia muziki yashuka kwa zaidi ya nusu
Kifaa maarufu cha kusikilizia muziki cha kampuni Apple, Ipod, ambacho kilisababisha kifo
cha kifaa cha kampuni ya Sony, Walkman – nacho kinakabiliwa na kifo chake chenyewe.
Kwa mujibu wa ripoti mpya ya hivi karibuni, Apple iliuza iPod milioni 6 kwenye robo ya
kwanza ya mwaka jana na kuonesha kuwa mauzo yameshuka kwa asilimia 52 ukilinganisha na
mwaka uliopita. Kwa sasa mauzo ya iPod yanaingiza asilimia 2 tu ya mapato ya kampuni ya
Apple.
Kushuka kwa mauzo ya vifaa hivyo yanadaiwa kutokana na kuongezeka kwa apps za muziki kwenye
simu, mitandao ya kuhifadhia muziki mtandaoni na kuchezea muziki kama Spotify. Kingine simu
za iPhones huja na iTunes na kufanya iPod zikose kazi kwa watumiaji wengi wa iPhone.
Mauzo ya iPod yalikuwa makubwa zaidi mwaka 2008 kufuatia kuanzishwa kwa iPod Touch mwishoni
mwa mwaka 2007. iPod Touch iliyotengenezwa kuonekana kama iPhone, ilikuwa ikicheza muziki na
kuwa na apps, lakini haikuweza kupiga simu.
source:bongo5
0 comments: