Oliver Kahn: Chelsea walinunua taji la ubingwa wa ulaya

172059_heroa
Gwiji wa soka wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani golikipa Oliver Kahn anaamini pesa sasa ndio inayoamua matokeo katika mchezo wa soka, akisisitiza kwamba namna Chelsea walivyoshinda ubingwa wa ulaya ni ushindi uliokuja baada ya matumizi makubwa ya fedha.
Klabu hiyo ya Premier League ilishinda taji hilo kubwa kabisa katika ngazi za soka barani ulaya katika upande wa vilabu mnamo mwaka 2012, miaka tisa baada ya kuwa chini ya bwana mapesa Roman Abramovich.
Kahn anaamini mafanikio ya Chelsea yanaonyesha kabisa kwamba fedha inaupeleka pabaya mchezo wa soka.
“Fedha imekuwa inaamua mambo mengi kwenye soka,” alisema golikipa huyo wa zamani Bavarians alipokuwa akiongea na jarida la Kicker.
“Ili kupanda daraja kucheza Bundesliga, unahitaji angalau bajeti ya kuanzia 20 mpaka 25 million euro. Kushinda  Champions League, unahitaji €300m.
“Abramovich alinunua taji lakini Chelsea haina na  Manchester City, Real Madrid, Barcelona au Bayern?”
Uefa wameleta sheria mpya ya udhibiti wa matumizi ya fedha za usajili ili kuzuia vilabu vikubwa vinaongozwa na matajiri kuutawala mchezo huu kwa msiuli yao ya fedha hivyo kupunguza ushindani.
source:milard ayo

0 comments: