KAMA WEWE NI BOSS AU UNAWAZO LA KUWA BOSS Yafahamu madhara ya bosi Mtata/Mkali

1. Kiafya
Kuripoti kwa bosi mtata au mbaya inakughalimu nguvu nyingi kuliko vile unavyofikiri kama 
unafanya kazi kwa masaa nane kwa siku au siku tano kwa wiki. Ukijikuta kwenye hali ngumu 
kikazi ,utakuwa na kazi mara mbili ili uweze kufanya kazi vizuri na vile vile kupambana na 
ukatili au unyanyasaji eneo hilo la kazi kitu ambacho utakifanya kwa muda wako.
Uwe makini mawazo yako au fikira zako zisikudanganye. Hakuna mtu ambaye anaweza 
kustahimili manyanyaso ya kifikra, na kisaikolojia kwa muda mrefu bila kukumbana na 
madhara kama, msongo wa mawazo, kushuka moyo, kushindwa kufanya kazi, kupoteza mwelekeo 
wa kile unachopaswa kufanya kazini, vilevile kupoteza uwezo na umakini wa kufanya jambo 
moja kwa muda mrefu. Haijalishi unajifanya unaweza kustahimili kwa muda mrefu, jitahidi 
manyanyaso ya bosi huyo mbaya au mtata yasiende zaidi ya wiki nne. Utakapokuwa na msongo 
wa mawazo, utapoteza nguvu nyingi ili upambane na hali hiyo. Jaribu kujitizama mwenyewe 
kama kuna dalili fulani kama hizo.
Kuwa makini kuwasikiliza ndugu na jamaa ambao mara nyingi wanakuuliza ;wewe tatizo ni nini? 
; unafikiri unaweza kutenga mambo ya kazi na maisha yako binafsi, bali ukishambuliwa 
kisaikolojia kama mabosi watata wanavyofanya mambo hayo yatakufuata kazini na nyumbani 
kutatokea madhara yake.Kama unafikiri ndani yako huhitaji msaada, labda hahuhitaji msaada 
lakini unahitaji msaada. Tafuta mwanasaikolojia ambaye atakusaidia kuongeza nguvu na uwezo 
wako kihisia ili kuboresha hali yako. 
 
 
 2  Kazi nyingi Haimaanishi majukumu zaidi
Mabosi watata au makatili au wabaya hunufaika na mazingira fulani kwa wafanyakazi, anakupa 
kazi nyingi zaidi ya zile unazohitajika kufanya badala ya kukuongezea majukumu ambayo 
yataweka changamoto katika utendaji wako. Na vile vile wanakuongezea majukumu bila kuongeza 
mshahara wako.
Kama wewe una majukumu ya kila siku na ukapewa kazi kubwa inayohitaji ujuzi zaidi na ni 
zaidi ya majukumu yako ya kazi kulingana na mkataba, unaweza kuwa unafanya kazi katika 
nyadhifa ya juu sana kuliko mshahara wako. Ingawa ukipewa jukumu kubwa ni fursa wa wewe 
kujifunza ujuzi mpya na inakuandaa katika hatua nyingine kubwa zaidi, hiyo inafaida kama; 
semina na mafunzo ya hapa na pale ambayo hayaendani na kuongezewa mshahara.
Kama bosi huyo ana mpango wa kukuendeleza kiutendaji, atakusaidia na kukuelekeza namna ya 
kufanikisha ila hata kuacha uhangaike nalo. Akikuacha ufanye mwenyewe halafu anataka 
matokeo mazuri huyo anampango wa kukuangusha. Kukuongezea majukumu kunaongeza uthamani 
wa kazi yako, na kwa muda fulani inaongeza faida ya kiwango cha mshahara kuongezeka na
 mambo mengine. 
 
 3.Pata nakala ya majukumu yako kikazi
Mshahara wako unatokana na majukumu yako na wajibu uliopewa kazini. Hivyo majukumu yako 
kikazi yanategemea ujuzi ulionao ambayo yameelezewa kwenye nakala ya majukumu unayotakiwa 
kufanya. Unapoyatekeleza yanatakiwa kulipwa kwa mshahara uliopangwa.
Nakala yako ya majukumu kikazi ni muhimu kuwa nayo. Majukumu hayo yanaelezwa bayana kwenye 
mkataba “kutoka siku hii, majukumu yako ni……… na utalipwa kiasi kadhaa” Hivyo usipokuwa na 
nakala ya majukumu yako, utakapoambiwa ufanye kazi fulani itakuwa ngumu kujua unatekeleza 
kulingana na vile utakavyolipwa au ni zaidi ya majukumu yako na kusababisha kutumiwa vibaya
 na mwajiri wako bila ya wewe kujua.
Ni haki yako kuomba nakala ya majukumu yako pale unapoanza kazi kabla changamoto hazijaanza 
kuibuka. Bosi wako asipokupatia kazitafute kwa afisa mwajiri, hasa kwa taasisi kubwa. Zile 
taasisi ndogo wanaweza wasiwe nazo ila waambie wakutengenezee na kukuandikia kuna wakati 
wanasema majukumu mengine kama utakavyopangiwa na bosi au msimamizi, tafuta kujua na 
wakwambie hayo majukumu mengine ili kujua yanaendana na kiwango cha mshahara wako?
Kumbuka kama haijaandikwa ni kwamba haipo

0 comments: