PICHA NA HABARI WAZIRI MKUU MSTAAFU SUMAYE ALIPOTEMBELEA CLOUDS FM
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye kuhusiana na urushaji wa matangazo kwa njia ya kisasa ndani ya studio kuu ya redio Clouds FM,Sumaye amefanya ziara fupi mjengoni humo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo zikiwemo na urushaji wa matangazo ya redio na Televisheni kwa ujumla.
Mmoja wa Watangazaji kipindii cha Michezo Clouds FM,kiitwacho Sports Extra, Ibrahim Masoud a.k.a Maestro akifanya mahojiano mafupi na Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye kuhusiana ushabiki wake mkubwa kwa timu ya Simba sambamba na migogoro iliyoikumba club hiyo ya Msimbazi
Ruge Mutahaba akitoa ufafanu mfupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye,kuhusiana na Kifaa maalum na cha kisasa cha kurushia matangazo ya biashara,pichani nyuma ni Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds FM,Joyce Shebe akisikiliza.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye akiwa kwenye chumba cha kurekodia mahojiano mbalimbali,akiwa amekutana na wadau wa Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT),pichani kulia ni Afisa Masoko Mwandamizi wa UTT,Mfaume Kimario na Afisa Masoko na Uhusiano,Bwa.Rahim Mwanga.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye kwenye moja ya Ofisi za kampuni hiyo,alipofanya ziara fupi mjengoni humo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo zikiwemo na urushaji wa matangazo ya redio na Televisheni kwa ujumla. pichani kati anaeshuhudia ni Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group,Simon Simalenga.
Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds FM,Joyce Shebe akitoa ufafanuzi mfupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye alipotembelea kitengo hicho cha habari na kujionea uandaaji wa habari ya televisheni na redio unavyofanyika.
Ruge Mutahaba akimtambulisha Mkurugenzi mwanzake wa Maendeleo ya Biashara,Sheba Kussaga kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye.
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM
0 comments: