PICHA:DK MAGUFULI AHAMIA MOROGORO KUSIMAMIA UJENZI DARAJA LA DUMILA LILILOSOMBWA NA MAJI

Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli akiwa katika gari linaloendelea na ujenzi wa daraja la Dumila.
Waziri Magufuli akitoa maelekezo kwa watendaji wa Tanroads.

Sehemu ya barabara iliyozolewa na maji ya mto Mkundi.
Waziri wa Ujenzi akikagua maeneo yaliyoharibika.
Dk. Magufuli akiendelea na kazi katika daraja hilo.
Kazi za ujenzi zikiendelea eneo hilo la daraja lililoharibika.
Dk. Magufuli akiwapa hi mafundi wanaoendelea na ujenzi wa daraja hilo.
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli amepiga kambi mkoani Morogoro kusimamia mwenyewe ujenzi wa Daraja la Dumila ambalo ni kiungo muhimu cha barabara ya Dodoma – Morogoro lililosombwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia tarehe 22.01.2014 na kusababisha magari kutopita kabisa ama yanayotoka upande wa Dodoma au Morogoro. Mbaya zaidi hakuna njia nyingine mbadala zaidi ya hiyo.
credit:boss ngasa

0 comments: