ALICHOKISEMA TUNDA MAN KUHUSU YEYE NA ROSE NDAUKA KATIKA MAHUSIANO
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tunda Man, amesema mpenzi wake wa
kwanza katika maisha yake ni mwanadada muigizaji wa filamu nchini Rose
Ndauka,ambaye waliachana tangu
2006.Akizungumza na XXL ya Clouds Fm Tunda amesema walikuwa wakikutana na
mwanadada huyo katika studio moja huko kariakoo hali iliyowapelekea
kuanza mahusiano yao yamapenzi.
“Kuna studio moja kariakoo,wanadada walikuwa wanakuja kuchana na yeye
anakuja studio anaangalia situation zinavyoenda, kwahiyo kuanzia hapo
ndiyo akaanza kunijua nini, nikaenda kwao kila kitu kikawa fresh kila
kitu kikawa kinaenda poa ni 2006 kitu kama hicho, yani tumeachana kabla,
hamna hata mmoja aliyekuwa star, sasa tumejikuta kila mmoja anafanya
issue zake na mimi nafanya issue zangu, mpaka sasa hivi nikikutana nae,
nasikia ameolewa peace tu ,kama na shida na yeye kwasababu na yeye sasa
hivi anapiga mapigo ya movie na mimi na movie zangu kama vipi
namdondosha halafu namlipa”, alisema Tunda
Credit:-Bongo5
0 comments: