Tattoo za wasanii wa bongo na maana zake
Kama tungekua nchi za wenzetu tukaanza kuandika kuhusu tatoo na wasanii basi tusingemaliza leo maana karibia kila msanii ana tatoo na sio moja tu bali zaidi ya moja.Lil Wayne ana zaidi ya tatoo 300 , Rihanna ana tatoo 19 ,Miley Cyrus ana tatoo 19 pia huku Bruno Mars akiwa na Tatoo 5 . Lakini vipi kwa upande wa bongo , Tatoo na usanii au umaarufu vimeanza kuendana hapa bongo na hii ni list ya wasanii wa bongo wenye tatoos.
Diamond Platnumz
Diamond ana tatoo kubwa kwenye mkono wake wa kulia maeneo ya begani na nyingine kwenye mkono wake wa kushoto yenye maandishi ya kichina ambayo maana yake ni “I love my mama”.
Wema Sepetu
Wema Sepetu ni moja kati ya wasanii wa bongo wenye tatoo nyingi , ana tatoo kwenye shingo yake , pia ana tatoo yenye maandishi ya kichina mgongoni yenye maana ya potential kwa kiingireza. pia ana tatoo mkononi na kwenye bega.
Ney wa Mitego
Ney wa Mitego ni mmoja kati ya wasanii wabishi wanaofanya muziki mgumu maarufu kama Hip Hop, ambaye amejaribu kubeba dhana hiyo kama msanii anayetafsirika kimwonekano. Ney wa mitego ameanza kuchora tatoo tokea mwaka 2002 alipokua kidato cha pili katika shule ya sekondari ya mbezi beach.Katika mkono wake wa kulia kuna tatoo yenye nanga ya hip-hop ikiwa na maana kuwa yeye ni mtu mwenye imani na ndoto za kufanikiwa kupitia muziki huo wa ‘Hip Hop’.‘tattoo’ iliyopo katika mkono wa kushoto ni nyoka mwenye mabawa(Dragon) ,kiumbe ambacho ni adimu kuonekana duniani.
Elizabeth Michael “Lulu”
lulu naye hayupo nyuma katika kuchora tatoo. kwa upande wa lulu ni kidogo na wengine kwani yeye ameambua kwenda straight forward na kuweka ujumbe wa maneno chini kidogo ya shingo lake karibia na bega unaosema “Only God can Judge Me”.
Jux
Jux ana tattoo mbili. Ya kwanza ipo kifuani na watu wengi wamekuwa wanasema tatoo hii inafanana na ile ya trey songs lakini ukweli ni kuwa sehemu ya mwili aliyoichorea ni kama ya Trey Songz lakini fonts na ujumbe ni tofauti kwani tattoo ya trey songz ameandika ameandika kwa ajili ya mama yake , mdogo wake wa kiume na bibi yake huku kwa upande wa jux ukiwa na ujumbe mzito pia lakini hatujajua bado unamhusu nani na part ya tattoo hiyo inasema “always missing you” na “hope to see you”. Jux ana tattoo nyingine mkononi maeneo ya bega ikiwa na “Virgo Angel” kwa kibongo tunaweza kuita mashuke .
Irene Uwoya
Uwoya nae ni kati ya wasanii wakubwa wakwanza kabisa kunyesha tatoo zake. ana tatoo juu kidogo ya matiti yake yenye alama ya nyayo za paka au chui.Pia ana tattoo mgongoni iliyoandikwa krrish ikiwa na alama za nyayo ya mtoto mdogo ambayo ni maalumu kwa mtoto wake Krrish Ndikumana.Kuna tattoo nyingine zinaonekana kiunoni na miguuni pia.
0 comments: