REAL MADRID YAINGIA KWENYE MBIO ZA KUMSAJILI ROONEY.
Taarifa kutoka jijini Madrid
zinasema mshambuliaji Wayne Rooney ameingia kwenye orodha ya washambuliaji
wanaowataka mwishoni mwa msimu.
Huku mkataba wa Rooney ukiwa umebaki
miezi 18 na inavyoelekea hana nia ya kuongeza mkataba mpya pia klabu ya Manchester Utd haipo tayari
kumuuza Rooney kwa vilabu vya England.
Kwenye orodha ya majina ya
washambuliaji wanaotakiwa na Real Madrid ukiacha jina la Rooney ni Radamel
Falcao na Kun Aguero
Sababu inayompa nafasi kubwa Rooney
kusajiliwa na Madrid ni uwezo wake kucheza nafasi mbali mbali ukiacha nafasi ya
ushambuliaji pia kocha wa sasa wa Madrid Carlo Anceletti anamfahamu vizuri
katika kipindi alichokuwa anaifundisha Chelsea.
Kama Rooney atafanikiwa kujiunga na
Madridi msimu ujao basi atajiunga tena na mshambuliaji Cristiano Ronaldo
waliyekuwa pamoja kwenye klabu ya Manchester Utd.
source:shafih dauda
0 comments: