Picha:mbalimbali ikiwemo ya Baa iliyo ndani ya ndege ya Emirates.
Mpaka mwaka 2010, wanasema Emirates walikua wanasafirisha abiria elfu mbili mia nne kwa wiki kutoka Dubai International Airport kwenda kwenye majiji 105 ndani ya nchi 62 duniani ambazo ziko ndani ya mabara sita.
Mpaka mwaka 2010 pia, Emirates walikua wameajiri Wafanyakazi elfu kumi na mia saba wanaotoka kwenye nchi mia moja ishirini duniani na kwenye kutimiza kwao miaka 25, walitangaza faida yao iliyofikia dola za kimarekani milioni 964.
Unaambiwa Terminal 3 kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Dubai ambayo ilianza kutumika mwaka 2008 baada ya kujengwa maalum kwa ajili ya kutumiwa na shirika hili la Emirates peke yake, iligharimu dola za Kimarekani bilioni 4.5 ikiwa ni jengo lililotajwa mwaka 2010 kuwa kubwa kwa kipimo cha upana likiwa na over 1,500,000 sq. m. (370 acres) of space.
Picha zinazofata hapa chini ndio zinaonyesha baa ambayo iko ndani ya Emirates Airline
source:milardayo.com
0 comments: