BARCELONA YATHIBITISHA KUTUMIA KIASI CHA PAUNDI MILIONI 495 KUUBORESHA UWANJA WA NOU CAMP.
Bodi ya wakurugenzi ya FC Barcelona
imekataa wazo la kujenga kiwanja kipya na badala yake wamekubaliana kuongeza
nguvu kuufanyia marekebisho uwanja wao wa Nou Camp.
Wanachama wa klabu ya FC Barcelona
ambao kimsingi ndio wamiliki wa timu hiyo watapewa nafasi ya kupitisha wazo hilo
la kuuboresha uwanja Wa Nou Camp kwa kupiga kura mnamo mwezi wanne mwaka huu
kwenye mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo.
Kama wazo hilo litapitishwa na
wanachama basi uwanja huo mkubwa kuliko viwanja vyote barani ulaya wenye uwezo
wa kuingiza mashabiki 98,000 kwasasa, utakuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki
105,000 na kusaidia kuongeza kipato kutokana na vyanzo vya uwanja huo.
Pia itakuwa fursa kwa mashabiki
kuweza kuwaona wachezaji nyota ulimwenguni kama vile Lionel Messi na Neymar.
Mradi huo ambao pia unahusisha
ujenzi wa kiwanja cha ndani cha mchezo wa kikapu pamoja na vitega ychumi
vingine vingi unataraji kuighalimu kiasi cha paundi milioni 495 ambazo ni sawa
na euro milioni 600.Kazi hiyo ya maboresho ya uwanja inataraji kuanza mwaka
2017 na inataria kumalizika mapema mwaka 2021.
Ili kufanikisha mradi huo Barcelona
inategemea kuchukua mkopo benki wa kiasi cha paundi milioni 165,pia inategemea
kupata kiasi cha paundi milioni 82 kutokana na haki za jina la uwanja huo na
kiasi kingine kilichobaki cha pesa kitatokana na vyanzo vilivyopo hivi sasa.
Raisi wa klabu hiyo Sandro Rosell
amesema wakati woote wa ujenzi michezo mbali mbali inayoihusu klabu hiyo
itaendelea kuchezwa kwenye uwanja huo.
0 comments: